• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China akutana na waziri mkuu wa Mauritius

    (GMT+08:00) 2018-07-29 08:20:58

    Rais Xi Jinping wa China ambaye yuko ziarani nchini Mauritius amekutana na waziri mkuu wa nchi hiyo Bw. Pravind Jugnauth.

    Rais Xi amepongeza mafanikio yaliyopatikana katika miaka 50 iliyopita tangu Mauritius ijipatie uhuru, na kusifu sera ya kirafiki kwa China inayotekelezwa na serikali za awamu mbalimbali za nchi hiyo. Pia amesema, China inapenda kuwa rafiki mkubwa na mwenzi mzuri wa Mauritius na kuhimiza kuinua uhusiano wa kirafiki na ushirikiano kati ya nchi hizo mbili kwenye kiwango cha juu zaidi.

    Bw. Jugnauth amemkaribisha tena rais Xi kupita Mauritius na kufanya ziara ya kirafiki na kihistoria nchini humo. Amesema Mauritius inaishuruku China kwa uungaji mkono na msaada wa muda mrefu, na inafuatilia maendeleo ya China kuingia katika zama mpya, huku akipongeza pendekezo la jumuiya yenye hatma ya pamoja ya binadamu lililotolewa na rais Xi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako