• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi amaliza ziara ya kwanza ya mwaka huu

    (GMT+08:00) 2018-07-29 10:12:22

    Kuanzia tarehe 19 hadi 29 Julai, Rais Xi Jinping wa China alifanya ziara nchini UAE, Senegal, Rwanda na Afrika Kusini, na kuhudhuria mkutano wa kumi wa viongozi wa nchi za BRICS, kufanya ziara ya kirafiki nchini Mauritius wakati akiwa njiani kurudi nyumbani. Hii ni ziara ya kwanza nje ya nchi kufanywa na rais Xi kwa mwaka huu. Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi amesema, hii ziara ya kihistoria yenye mafanikio ambayo inaimarisha ushirikiano wa kimkakati kati ya China na nchi zinazoendelea pamoja na nchi zinazojitokeza kiuchumi.

    Katika ziara yake ya siku 11, rais Xi ametembelea sehemu 6 za nchi tano na kuhudhuria shughuli 60 hivi kati ya pande mbili au nyingi. Bw. Wang amesema, ziara yake inafungua ukurasa mpya kwa sera ya diplomasia ya nchi kubwa yenye sifa ya China, ambayo pia imeanzisha hali mpya ya uhusiano kati ya China na nchi za nje na ushirikiano kati ya nchi zinazoendelea. Mbali na hayo, ziara hiyo pia imepanua nafasi mpya ya maendeleo ya ndani na utekelezaji wa mikakati na kuhimiza utekelezaji mpya wa kujenga jumuiya yenye hatma ya pamoja ya binadamu.

    Bw. Wang pia amesema, huu ni mwaka muhimu sana kwa maendeleo ya uhusiano kati ya China na Afrika. Baada ya ziara ya rais Xi barani Afrika, mkutano wa kilele wa FOCAC utafanyika mwezi wa Septemba hapa Beijing. Mkutano huo utaunganisha pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja", ajenda za maendeleo endelevu ya mwaka 2030 zilizotolewa na Umoja wa Mataifa, ajenda ya mwaka 2063 iliyotolewa na Umoja wa Afrika, pamoja na mikakati ya maendeleo ya nchi mbalimbali, ili kutoa njia mpya ya kuimarisha ushirikiano wa pande zote kati ya China na Afrika. Rais Xi amejulisha wazo la kuandaa mkutano huo wakati akifanya ziara barani Afrika, viongozi wa nchi za Afrika wamesema wanapenda kushirikiana na China, kuufanya mkutano huo kuwa shughuli nyingine ya kihistoria ya kuimarisha ushirikiano na mshikamano kati ya China na Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako