• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Ulaya hauna uwezo wa kuisaidia Marekani kukwamua hali ya soko la soya

    (GMT+08:00) 2018-07-29 16:41:47

    Kwenye mkutano wa kisiasa uliofanyika tarehe 26 kwenye jimbo la Iowa, rais Donald Trump wa Marekani alitangaza kwa furaha kuwa, serikali ya Marekani imefungua mlango wa Ulaya kwa wakulima wa Marekani, na wakulima wa Marekani watakuwa na soko kubwa.

    Siku hiyo hiyo, mjumbe wa biashara wa Marekani Bw. Robert Lighthizer kwenye bunge la Marekani alisema Marekani inafanya mazungumzo na Ulaya kuhusu suala la kilimo. Lakini maofisa wa Umoja wa Ulaya walisema kilimo si mada ya mazungumzo kati ya Ulaya na Marekani, walizungumzia mambo yaliyokuwa yemepangwa na taarifa ya pamoja tu.

    Msemaji wa Umoja wa Ulaya Bi. Mina Andreeva alisema, taarifa ya pamoja iliyotolewa na Marekani na Ulaya haikutaja kilimo, lakini ilitaja wakulima na soya, ambavyo ni sehemu ya mada ya mazungumzo.

    Lakini je, Umoja wa Ulaya una uwezo wa kuisaidia Marekani kukwamua hali ya soya? Shirika la habari la Bloomberg lilisema hapana. Ripoti iliyotolewa na shirika la Bloomberg inasema, mwaka jana China iliagiza soya zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 12.3 kutoka Marekani, na thamani ya uagizaji wa soya ya Umoja wa Ulaya kutoka Marekani ilifikia dola za kimarekani bilioni 1.6 tu. Umoja wa Ulaya hauwezi kusuluhisha hasara ya wakulima wa Marekani kutokana na vita ya biashara iliyofanywa na serikali ya Marekani dhidi ya China, na shinikizo la kisiasa dhidi ya rais Trump na wabunge wa chama cha GOP kutoka majimbo ya kilimo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako