• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkoa wa Xinjiang wawavutia wahariri waandamizi kutoka nje ya nchi

    (GMT+08:00) 2018-07-29 16:44:51

    Ziara ya siku tano kwenye mkoa wa Xinjiang kaskazini magharibi mwa China imewavutia kwa kiasi kikubwa wahariri waandamizi 23 kutoka vyombo vya habari vya nchi 18 tofauti zikiwemo Misri, India, Pakistan, Kyrgyzstan na Saudi Arabia.

    Miongoni mwa walioelezwa kuvutiwa ni Musallam al-Dawsri ambaye ni mhariri mkuu wa gazeti moja la mtandaoni nchini Saudi Arabia, yeye amesema maendeleo aliyoyaona Xinjiang hakuwahi kuyafikiria, hivyo sasa anajiamini kuwa anaweza kuandika na kuieleza dunia mengi zaidi kuhusu eneo hilo la Kaskazini Magharibi ya China.

    Ziara hiyo ni sehemu ya semina maalum iliyoandaliwa na Idara kuu ya mawasiliano na habari ya China, iliyoanza Julai 21 hadi 25 ambapo walitembelea maeneo mengi, ikiwemo Beijing baada ya kukamilisha ziara ya Xinjiang.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako