• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Misri awahimiza waisraeli kutumia "fursa kubwa" ya sasa kutimiza amani

    (GMT+08:00) 2018-07-30 08:47:30

    Rais Abdel-Fattah al-Sisi wa Misri amewahimiza watu wa Israel kutumia fursa kubwa inayopatikana kutimiza amani kati yao na wapalestina.

    Rais al-Sisi amesema hayo akijibu maswali kwenye mkutano wa siku mbili wa vijana uliofanyika katika chuo kikuu cha Cairo. Amesema kuna fursa ya kupata amani na utulivu kwenye kanda hiyo kupitia kutafuta ufumbuzi wa suala hilo, ambao hautatishia usalama na utulivu wa Israel.

    Akizungumzia mpango wa utatuzi unaoungwa mkono wa Marekani, rais Al-Sisi amesisitiza msimamo thabiti wa Misri wa kuunga mkono kuanzishwa kwa nchi huru ya Palestina yenye mipaka iliyoamuliwa mwaka 1967, na Jerusalem mashariki kuwa mji mkuu wake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako