• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maelfu ya waethiopia wamiminika kuaga mwili wa mhandisi wa bwawa la GERD la Ethiopia

    (GMT+08:00) 2018-07-30 09:14:42

    Maelfu ya wananchi wa Ethiopia wamemiminika kuuaga mwili wa mhandisi mkuu wa bwawa la GERD la Ethiopia Bw Simegnew Bekele, aliyeuawa alhamisi kwa kupigwa risasi mjini Addis Ababa.

    Mpaka sasa polisi wa Ethiopia hawajasema kama kifo chake kinatokana na kujipiga risasi au alipigwa risasi. Maelfu ya waethiopia ikiwa ni pamoja na Rais wa nchi hiyo Bw Mulatu Teshome, waljitokeza kuaga mwili wake ambao uliopumzishwa katika kanisa kuu la ki-orthodox.

    Bw. Bekele alikuwa mhandisi mkuu wa bwawa la GERD lilioanza kujengwa mwaka 2011 kwenye mto Blue Nile, na sasa ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 66.

    Waziri mkuu wa Ethiopia Bw. Abiy Ahmed amesema anaamini kuwa Bw. Bekele aliuawa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako