• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uchaguzi mkuu wafanyika nchini Zimbabwe

    (GMT+08:00) 2018-07-30 16:35:18

    Wananchi wa Zimbabwe wamepiga kura leo katika uchaguzi wa kwanza wa rais tangu aliyekuwa rais wa nchi hiyo Robert Mugabe ajiuzulu mwezi Novemba mwaka jana.

    Zoezi la upigaji kura lilianza saa moja asubuhi kwa saa za huko na lilitarajiwa kumalizika saa moja usiku. Misururu mirefu ilionekana mapema asubuhi nje ya vituo vya kupigia kura katika eneo la Bustani ya Warren. Baadhi ya wapiga kura wamesema walianza kupanga foleni tangu alfajiri, na wanachohitaji kutoka kwa serikali mpya ni ajira, kumaliza mgogoro wa kifedha, na kuboresha huduma za afya.

    Rais wa sasa wa nchi hiyo Emmerson Mnangagwa anagombea nafasi hiyo na watu wengine 22, huku mpinzani wake mkubwa akiwa ni Nelson Chamisa, kiongozi wa muungano wa upinzani wa MDC.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako