• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 15 watekwa nyara kaskazini magharibi mwa Nigeria

    (GMT+08:00) 2018-07-30 19:06:54

    Wanakijiji 15 wametekwa nyara na watu wenye silaha ambao walishambulia kijiji cha Maradun kilichoko jimbo la Zamfara, kaskazini magaribi mwa Nigeria mwishoni mwa wiki iliyopita.

    Spika wa bunge la jimbo hilo Sanusi Rikiji ameliambia Shirika la Habari la China Xinhua kuwa mateka hao hawajulikani walipo, na kuongeza kuwa, hivi karibuni, vijiji na miji 18 katika wilaya tatu za mkoa huo zimeshuhudia mashambulizi ya mara kwa mara yanayofanywa na watu wenye silaha.

    Jana, serikali ya Nigeria ilitangaza kupeleka wanausalama zaidi ya 1000 ili kukabiliana na mashambulizi katika jimbo hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako