• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kampuni zaidi ya 2,800 kushiriki kwenye Maonyesho ya kwanza ya Kimataifa kuhusu bidhaa zinazoagizwa kutoka nje nchini China

    (GMT+08:00) 2018-07-30 20:30:04

    Kampuni zaidi ya 2,800 kutoka nchi na sehemu zaidi ya 130 duniani zimethibitisha kushirika katika Maonyesho ya kwanza ya Kimataifa ya China ya bidhaa zinazoagizwa kutoka nje.

    Naibu waziri wa biashara wa China Bw. Wang Bingnan pia amesema, nchi 80 na mashirika matatu ya kimataifa yamethibitishwa kushirika katika maonyesho ya biashara na uwekezaji ya kimataifa. Amesema takwimu za awali zimeonyesha kwamba kampuni zitakazoshiriki katika maonesho hayo zitataleta bidhaa na teknolojia mpya zaidi ya 100 ili kuonyesha bidhaa na huduma za kisasa na zenye kiwango cha juu. Nchi zaidi ya 70 zitakazoshiriki kwenye maonyesho hayo zimethibitisha vitu vitakavyooneshwa ambavyo vitahusisha biashara ya bidhaa, utoaji wa huduma, viwanda, uwekezaji na utalii, pamoja na bidhaa zenye umaalumu wa nchi husika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako