• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • matumizi ya maendeleo yamepungua kwa Sh bilioni 23 kutoka Sh billion 62

    (GMT+08:00) 2018-07-30 20:59:24

    Uchunguzi na Mdhibiti wa Bajeti Agnes Odhiambo amesema matumizi ya fedha katika kaunti inaendelea kuongezeka kwa upande wa mishahara na safari za kigeni huku sekta ya maendeleo ikiendelea kuumia.

    Katika kipindi cha ukaguzi, matumizi ya maendeleo yamepungua kwa Sh bilioni 23 kutoka Sh billion 62 zilizotumika kwa kipindi kama hicho mwaka wa fedha wa 2016-2017.

    Ripoti ya Odhiambo inaonyesha Garissa, Kirinyaga na Kisumu hawakutumia fedha yoyote katika maendeleo hata baada ya kuongeza matumizi yao kwa safari za ndani na za kigeni, hasa kati ya mwezi Julai 2017 na Machi 2018.

    Odhiambo amesema matumizi makubwa kwa mishahara yanaweza athiri vibaya maendeleo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako