• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Uganda alaani uamuzi wa mahakama kupiga marufuku kurefusha muda wa ubunge na udiwani

    (GMT+08:00) 2018-07-31 09:14:34

    Rais Yoweri Museveni wa Uganda amesema uamuzi wa hivi karibuni wa mahakama ya katiba kuzuia kurefushwa kwa muda wa ubunge na udiwani si wa kidemokrasia, kwa kuwa majaji wa mahakama hiyo walizingatia mchakato na sio maana ya uamuzi huo.

    Julai 26 majaji watano wa mahakama ya katiba walisema hatua zilizofuatwa kwenye kurefusha muda wa bunge na mabaraza ya madiwani ulifikiwa kimakosa na bunge, kwa kuwa wabunge hawakuwasiliana na watu wanaowawakilisha.

    Rais Museveni amesema wabunge wa chama chake cha NRM wako karibu sana na wananchi, na mabadiliko ya katiba yanaweza kufanyika kwa kuwashirikisha au kutowashirikisha majaji.

    Hata hivyo Rais Museveni alikubaliana na uamuzi wa mahakama hiyo kukubali kuwa kuondoa ukomo wa umri wa kugombea urais, hakukiuki katiba.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako