• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya na Ethiopia kukamilisha kuunganisha umeme kati yao katikati ya mwaka kesho

    (GMT+08:00) 2018-07-31 09:15:15

    Katibu mkuu wa wizara ya nishati ya Kenya Bw. Joseph Njoroge, amesema kiunganisho cha umeme kati ya Kenya na Ethiopia kimepangwa kukamilika katikati ya mwaka 2019.

    Akiongea jana mjini Nairobi Bw. Njoroge amesema nyaya zenye urefu wa kilometa 1,045 zimekamilika kwa asilimia 70 kutoka upande wa Kenya na asilimia 90 upande wa Ethiopia.

    Mradi wa kuunganisha umeme kati ya Kenya na Ethiopia, wenye kilometa 612 za nyaya kwa upande wa Kenya, na kilometa 433 kwa upande wa Ethiopia unajengwa kwa fedha za benki ya maendeleo ya Afrika.

    Amesema mradi huo ni sehemu ya mradi wa umeme wa nchi za Afrika Mashariki wenye lengo la kusambaza umeme kwenye nchi za Afrika Mashariki, kutoka kwenye nchi zenye umeme wa ziada kwenda kwenye nchi zenye upungufu wa umeme.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako