• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la Usalama la UM lajadili uwezekano wa kuondoa vikwazo dhidi ya Eritrea

    (GMT+08:00) 2018-07-31 10:11:09

    Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linajadili uwezekano wa kuondoa vikwazo dhidi ya Eritrea kufuatia maendeleo yaliyopatikana.

    Hayo yamesemwa na balozi wa Sweden kwenye Umoja wa Mataifa Bw. Olof Skoog, ambaye nchi yake ni mwenyekiti wa zamu wa Baraza la Usalama kwa mwezi Julai, baada ya mkutano wa ndani wa Baraza hilo kuhusu Eritrea na Somalia.

    Balozi huyo amesema nchi wanachama zimezipongeza Eritrea na Somalia kwa kutangaza kushirikiana kuleta amani na utulivu wa kikanda, na wamesisitiza utayari wao wa kuunga mkono juhudi hizo.

    Akizungumzia kama Baraza hilo litaondoa vikwazo dhidi ya Eritrea, balozi Skoog amesema majadiliano kuhusu suala hilo yanafanyika, na Baraza la Usalama linapenda kusaidia juhudi zinazoweza kutatua suala hilo.

    Ethiopia imeomba kuondolewa kwa vikwazo dhidi ya Eritrea baada ya nchi hizo mbili kusaini Azimio la Amani na Urafiki tarehe 9, Julai na kukubaliana kurejesha uhusiano wa nchi mbili kwenye hali ya kawaida. Ethiopia pia imeeleza kupenda kuzisaidia Eritrea na Djibouti kutatua mgogoro wao wa mpaka, ili uhusiano wa nchi hizo pia urudi katika hali ya kawaida.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako