• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Riadha, Ubingwa wa Afrika: Timu zawasili nchini Nigeria, michuano kuanza kesho

    (GMT+08:00) 2018-07-31 10:19:29

    Timu zinazoshiriki mashindano ya ubingwa wa riadha barani Afrika (Afrika Athletics Championship) kwa mwaka huu zimeanza kuwasili nchini Nigeria kwa ajili ya michuano hiyo inayotarajiwa kuanza kesho mjini Asaba.

    Licha ya kutotangazwa sana michuano huyo mikubwa imekuwa na mvuto hasa baada ya mataifa yanayosifika kwenye medani za riadha kimataifa kushiriki.

    Miongoni mwa nchi zinazoshiriki mashindano hayo ambayo ni ya 21 tangu kuanzishwa kwake ni Kenya, Nigeria, Ethiopia, Sudan, Uganda, Tanzania na Ivory Coast.

    Mwaka jana mashindano kama hayo yalifanyika nchini Afrika Kusini na washindi wa jumla walikuwa ni wenyeji Afrika Kusini walipojizolea medali nyingi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako