• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yazindua mpango wa kuhimiza uuzaji nje wa bidhaa ili kupunguza urari mbaya wa biashara

    (GMT+08:00) 2018-08-01 09:04:09

    Serikali ya Kenya imezindua mpango wa kuhimiza uuzaji wa bidhaa nje ya nchi, ili kupunguza pengo la urari mbaya wa biashara linalozidi kuongezeka.

    Naibu Rais wa Kenya Bw. William Ruto amesema mjini Nairobi kuwa mpango huo unaohusu kupanua uuzaji nje wa bidhaa, ili kufikia urari mzuri wa biashara katika kipindi cha kati. Bw Ruto amesema mpango huo utaisaidia Kenya kuuza nje bidhaa kutoka thamani sawa na asilimia 8 ya pato la ndani hadi kufikia asilimia 25 kabla ya mwaka 2022.

    Ametaja sekta nane zitakazotiliwa mkazo ni pamoja na nguo, kilimo, mifugo, uvuvi, mafuta na gesi, madini na sanaa za mikono.

    Kwa mujibu wa takwimu za serikali, mwaka jana Kenya iliagiza bidhaa zenye thamani ya dola bilioni 17, na kuuza bidhaa zenye thamani ya dola bilioni 6.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako