Watu zaidi ya 17 wameuawa na wengine kadhaa wamejeruhiwa na mamba katika kingo za mto Zigi wilaya ya Muheza, kaskazini mashariki mwa Tanzania tangu mwezi wa Januari.
Ofisa wa misitu wa wilaya ya Muheza Bibi Jane Madega amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo na kuwalaumu wanavijiji kwa kupuuza onyo la serikali kuwa mbali na mto huo.
Bibi Madege amesema wamewataka watu kutokaribia ndani ya mita 60 na mto Zigi, ili kuepuka mamba, na kutokwenda kinyume cha sheria ya ulinzi wa mazingira.
Mbunge wa Muheza Bw. Adadi Rajabu pia amethibitisha kuwa vifo vingi vilitokana na mashambulizi ya wanyama hao wakati watu wakichota maji katika mto Zigi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |