• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mawaziri wa mambo ya nje wa China na Malaysia wakutana Kuala Lumpur

    (GMT+08:00) 2018-08-01 10:05:35

    Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi amekutana na mwenzake wa Malaysia Bw. Saifuddin Abdullah mjini Kuala Lumpur.

    Bw. Wang amesema China na Malaysia zina urafiki mkubwa wa jadi, na zote ni nchi zinazoendelea, na maslahi ya pamoja ya pande hizo mbili ni makubwa kuliko migongano. Amesema China inatilia maanani ushirikiano kati yake na Malaysia na itaendelea kushikilia sera ya kirafiki kwa Malaysia, na kuzidisha ushirikiano wa kunufaishana, ili kuwanufaisha watu wa nchi hizo mbili.

    Bw. Saifuddin amesema Malaysia inaichukulia China kama jirani mwema na mwenzi muhimu, serikali mpya ya nchi hiyo inatilia maanani uhusiano kati yake na China. Pia amesema Malaysia itaunga mkono na kushiriki kwenye ujenzi wa pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja".

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako