• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Timu zaanza maandalizi kwa ajili ya msimu mpya wa ligi kuu

    (GMT+08:00) 2018-08-01 11:23:41
    Kocha wa muda wa timu ya SC Villa ya Uganda Moses Basena amekiri ugumu wa kazi ya kuleta mafanikio, hasa ushindi.

    Basena ambaye amewahi kuwa mchezaji wa klabu hiyo na amewahi kuwa kocha msaidizi mwanzoni mwa miaka ya 2000 chini ya kocha Micho, sasa amekabidhiwa jukumu la kuifundisha timu hiyo katika kipindi cha mpito.

    Tayari kocha huyo ameanza kazi, na klabu imekubali maoni yake ya kufanya usajili wa wachezaji ili kuimarisha timu kwa ajili ya msimu ujao wa soka.

    Msimu uliopita Villa ilimaliza katika nafasi ya 3 kwenye msimamo wa ligi ikiwa nyuma ya mabingwa Vipers FC na washindi wa pili KCCA.

    Mtihani wa kwanza kwa Basena katika kuiongoza timu hiyo utakuwa kwenye mechi ya michuano ya 8 bora dhidi ya Police FC.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako