• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Benki kuu ya Marekani yaamua kudumisha viwango vya riba vya sasa

    (GMT+08:00) 2018-08-02 08:47:17

    Benki kuu ya Marekani imeamua kutobadilisha viwango vya riba, wakati mgogoro wa kibiashara kati ya Marekani na washirika wake wa biashara unaendelea.

    Taarifa iliyotolewa na benki hiyo baada ya mkutano wa siku mbili inasema soko la ajira nchini Marekani limeimarika, shughuli za kiuchumi zimeongezeka kwa kiwango kikubwa, na kiwango cha mfumuko wa bei kiko karibu na asilimia mbili, ambayo ni lengo la benki hiyo. Mkuu wa benki hiyo Bw. Jerome Powell amesema athari za sera ya biashara ya serikali ya rais Trump bado hazijaonekana kwenye takwimu, licha ya wasiwasi kuwa sera hiyo italeta athari hasi kwa uchumi wa Marekani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako