• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaahidi kupanua uhusiano na serikali ijayo ya Zimbabwe

    (GMT+08:00) 2018-08-02 09:08:21

    China imepongeza uchaguzi mkuu uliofanyika kwa amani nchini Zimbabwe, na kueleza nia yake ya kupanua uhusiano na serikali ijayo ya Zimbabwe kwa ajili ya maslahi ya nchi hizo mbili.

    Akizungumza na wanahabari mjini Harare, mkuu wa timu ya waangalizi ya China Bw Liu Guijin amesema upigaji kura uliofanyika kwa amani na uaminifu, utahimiza uwekezaji wa China nchini Zimbabwe.

    Uchunguzi unaonyesha kuwa chama tawala cha ZANU-PF kinachoongozwa na rais Emmerson Mnangagwa kimepata kura nyingi ziadi, na matokeo ya mwisho ya uchaguzi wa urais yanatarajiwa kutangazwa tarehe 4 mwezi huu.

    Wakati huo huo, wafuasi wa vyama vya upinzani jana walipambana na polisi mjini Harare, ambako watu watatu wameuawa na wengine wengi wamejeruhiwa. Msemaji wa polisi Bibi Charity Charamba amewaonya viongozi wa kundi la upinzani MDC Alliance kutochochea vurugu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako