• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya kuandaa kongamano la kufufua mazingira ya Afrika mwishoni mwa mwezi huu

    (GMT+08:00) 2018-08-02 10:10:29

    Zaidi ya watu 800 wakiwa ni pamoja na wanasiasa, wanasayansi na wanamazingira watakutana na kujadiliana kuhusu kutafuta njia za kufufua mazingira yaliyoharibika barani Afrika, kwenye kongamano litakalofanyika mwishoni mwa mwezi huu mjini Nairobi, Kenya.

    Kongamano hilo la siku mbili litakaloandaliwa na Taasisi ya uchunguzi wa misitu CIFOR, Shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP na Benki ya dunia, linalenga kufuatilia uharibifu wa mazingira na misitu unaotokana na shughuli za binadamu na mabadiliko ya hali ya hewa.

    Mkurugenzi mkuu wa CIFOR Bw. Robert Nasi, amesema ni lazima kurejesha mazingira mazuri ya Afrika ili kukidhi mahitaji ya raslimali yanayoendelea kuongezeka. Washiriki wa kongamano hilo watajadili hatua zenye ufanisi za kufufua mazingira, ili kuimarisha usalama wa chakula na kupunguza umaskini na migogoro ya kugombea raslimali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako