• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Njama ya Trump ya kuihujumu China inapoteza ufuatiliaji

    (GMT+08:00) 2018-08-03 09:03:52

    Mwakilishi wa biashara wa Marekani Bw. Robert Lighthizer alitangaza jumatano kuwa rais Donald Trump wa Marekani amemwagiza kupandisha kiwango cha ushuru kwa bidhaa za China zenye thamani ya dola bilioni 200 za kimarekani, kutoka asilimia 10 hadi kufikia asilimia 25, ikiwa ni hatua nyingine ya serikali ya Trump ya kuilazimisha China kufanya mabadiliko.

    Wafanya maamuzi wa Marekani wanaona hatua hiyo nzito itazusha mjadala mkubwa kwenye jumuiya ya kimataifa, lakini safari hii imewasononesha, kwa kuwa hata vyombo vikubwa vya habari vya Marekani havikufuatilia habari hiyo.

    Kinachostahili kufuatiliwa ni kwamba, kwa upande mmoja Marekani inatangaza wazi kuwa itaongeza ushuru dhidi ya bidhaa za China, kwa upande mwingine inatoa habari kuwa inataka kurejesha mazungumzo na China.

    Kuhusu hali hiyo, wizara ya biashara ya China imesema Marekani inacheza mchezo wa "vitendo vikali na kauli tamu" na China, bila kujali maslahi ya dunia nzima, na hata kutojali maslahi ya wakulima, wafanyabiashara na wateja wa Marekani, vitendo ambavyo havitafanikiwa kwa China, na vitazikatisha tamaa nchi na sehemu mbalimbali duniani zinazopinga vita ya biashara.

    Katika miezi minne iliyopita tangu Marekani ilipoanzisha vita ya biashara dhidi ya China, hatua zinazochukuliwa na Marekani zimeharibia sifa yake yenyewe, na mchezo wa rais Trump unapoteza watazamaji duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako