• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya na Umoja wa mataifa kushirikiana kupunguza tatizo la kuongezeka kwa matumizi ya dawa za kulevya

    (GMT+08:00) 2018-08-03 09:20:00

    Serikali ya Kenya inapanga kushirikiana na ofisi ya umoja wa mataifa ya kupambana na uhalifu na dawa za kulevya, wanapanga kushirikiana kupambana na matumizi ya dawa za kulevya yanayozidi kuongezeka.

    Mwenyekiti wa mamlaka ya taifa ya kupambana na dawa za kulevya ya Kenya NACADA Bw. Julius Githiri amewambia waandishi wa habari kuwa kupanuka kwa kasi kwa miji ya Kenya kunaleta kuharibika kwa mfumo wa jamii na kusababisha ongezeko la matumizi ya dawa za kulevya.

    Kwa mujibu wa NACADA, mwaka jana wakenya milioni 4.9 walitumia dawa za kulevya, na dawa zilizotumika zaidi ni bangi, Cocaine na Heroine. Tayari Ofisi ya umoja wa mataifa ya kupambana na uhalifu na dawa za kulevya inaendesha mpango wa kuelimisha watu kukabiliana na tatizo hilo, kwenye mkoa wa pwani ambao ndio una matumizi makubwa ya dawa za kulevya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako