• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu mkuu wa UM afurahia matokeo ya mkutano wa kilele wa kanda za Afrika

    (GMT+08:00) 2018-08-03 09:29:13

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw Antonio Guterres amepongeza matokeo yaliyopatikana kwenye mkutano wa kilele wa kanda za kati na magharibi mwa Afrika.

    Naibu msemaji wa umoja wa mataifa Bw Farhan Haq ametoa taarifa akisema Bw Guterres amefurahia kuona kwamba nchi wanachama wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi na nchi wanachama wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika ya kati, zimeahidiana tena kuimarisha ushirikiano ili kukabiliana kwa pamoja na changamoto za amani na usalama.

    Taarifa imesema Bw. Guterres ameamua kusaini makubaliano ya ushirikiano wa kijinai ndani ya mwaka huu, na kuunda tume ya mawaziri ili kusimamia utekelezaji wa matokeo ya mkutano wa kilele.

    Bw Guterres pia amefurahia uamuzi wa kufanya mkutano kila baada ya miaka miwili kati ya viongozi wa nchi za kanda hizo mbili, ili kupitia utekelezaji wa Azimio la Lome lililofikiwa kwenye mkutano wa kilele.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako