• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • DRC kuimarisha ushirikiano na Angola

    (GMT+08:00) 2018-08-03 09:54:03

    Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC ameeleza matumaini yake ya kuimarisha ushirikiano kati ya nchi yake na Angola. Rais Kabila aliwasili mjini Luanda kwa ziara rasmi na ya kikazi kutokana na mwaliko wa rais Joao Lourenco wa Angola.

    Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, rais Joseph Kabila ameeleza matumaini ya kuzidisha uhusiano katika sekta za biashara na miundombinu kati ya nchi hizo mbili. Pia amesisitiza kuwa masuala yaliyojadiliwa kwenye mazungumzo kati yake na rais Lourenco yanaweza kusaidia kuimarisha ushirikiano, haswa katika usalama wa mpakani, ili kuwanufaisha watu wa nchi mbili.

    Taarifa iliyotolewa na Ikulu ya Angola imesema ziara hiyo imekuja kutokana na urafiki na ushirikiano kati ya nchi mbili na mawasiliano ya kawaida kati ya wakuu hao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako