• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zambia yatoa wito wa juhudi za pamoja kutatua magendo ya binadamu Kusini mwa Afrika

    (GMT+08:00) 2018-08-03 09:55:55

    Serikali ya Zambia imetoa wito wa juhudi za pamoja kutatua suala la magendo ya binadamu katika kanda ya kusini mwa Afrika.

    Wito huo umetolewa kufuatia kuokolewa kwa wasichana sita na mvulana mmoja wa Zambia kutoka Namibia, ambako wanadaiwa kusafirishwa kufanya kazi kama ukahaba na uyaya.

    Vijana hao kutoka sehemu ya magharibi ya Senanga waliokolewa kutokana na ushirikiano kati ya polisi wa Zambia na Namibia.

    Katibu wa kudumu wa wizara ya jinsia ya nchi hiyo Bibi Auxilia Ponga, amesema suala hilo linahitaji kutatuliwa kwa juhudi za pamoja wakati wasichana wako hatarini kuwa wahanga wa magendo ya binadamu kutokana na kuwa rahisi kulazimishwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako