• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • WHO yathibitisha kuwa ugonjwa wa Ebola umetokea tena nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo

    (GMT+08:00) 2018-08-04 18:13:41

    Shirika la afya duniani WHO, jana lilithibitisha rasmi kuwa ugonjwa wa Ebola umetokea kwenye mkoa wa Kivu, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Shirika hilo lilikadiria kuwa idadi ya wagonjwa huenda ikaongezeka katika wiki zijazo. Naibu mkurugenzi wa shirika hilo Dr.Peter Salama alisema kuwa, uchunguzi wa kutokea kwa ugonjwa huo uko katika kipindi cha kwanza, licha ya wagonjwa 4 waliothibitishwa kuambukizwa ugonjwa wa Ebola, wengi wa wagonjwa bado wanachunguzwa. Watu 20 wamekufa lakini hivi sasa bado haiwezekani kuthibitishwa endapo sababu ya vifo vyao inahusiana na virusi vya Ebola au la.

    Mwezi Mei mwaka huu, ugonjwa wa Ebola ulitokea kwenye mkoa wa Ikweta, kaskazini magharibi mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, na kusababisha vifo vya watu 33. WHO ilitumia mfuko wa dharura wa dola za kimarekani milioni 4 na kukusanya dola za kimarekani milioni 63 pamoja na washirika kukinga na kudhibiti ugonjwa huo. Tarehe 24 mwezi Julai, shirika la hilo na serikali ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo zilitangaza kumalizika kwa ugonjwa huo nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako