• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kauli ya Lawrence Kudlow inakanganya Marekani

    (GMT+08:00) 2018-08-04 19:05:25

    Mkurugenzi wa kamati ya uchumi ya Marekani Lawrence Kudlowameongea na baadhi ya vyombo vya habari na kuonya CHina kutopuuza uwezo wa rais Trump wa kutimiza ahadi yake, na kusema Marekani itaunda muungano kwa haraka kukabiliana na kitendo kisicho cha haki cha biashara ya China.


    Bw. Kudlow amesema, hivi karibuni Marekani na Ulaya zimeanza kujadili kufikia makubaliano ya biashara, na inakadiria kuwa itafikiana na Mexico haraka. Pia anaona kuwa, Marekani itaunda muungano wa kutoa shinikizo kwa China juu ya kitendo chake kisicho cha haki.


    Kuunda muungano huo hakuendana na hali halisi, hasa tunaweza kusema inakanganya Marekani. Kwa maoni yake, mazungumzo magumu yanayoendelea miaka mingi yanaweza kukamilisha ndani ya wiki kadhaa. Mazungumzo kati ya Marekani na Umoja wa Ulaya yataanzisha hivi karibuni, lakini yanakabiliana na matatizo yaani suala la kilimo. Ufasansa imesema haitafanya mazungumzo na Marekani kuhusu suala la kilimo, Marekani inataka Umoja wa Ulaya kufungua soko la kilimo haiwezekani.

    Mexico katika miaka ya hivi karibuni inajitahidi kuimarisha biashara na China ili kupunguza utegemezi wake kwa Marekani. Canada kutokana na vita ya biashara kati yake na Marekani, haijashiriki kwenye mazungumzo ya eneo ya biashara huria ya Amerika ya Kaskazini. Kwa hivyo Kudlow kutaka Canada kujiunga na muungano wa kutoa shinikizo kwa China, kunahitaji muda.
    Kama China, Marekani, Umoja wa Ulaya Japan na makundi mengine muhimu la uchumi kukaa pamoja kujadili kuhusu mageuzi ya lazima ya WTO, ili kuhakikisha uendeshaji wa kawaida wa mfumo wa biashara wenye pande nyingi duniani, na kuufanya mgogoro wa kibiashara utatuliwe kwa ufanisi ndani ya WTO, dunia nzima itafaidika. Huo ndio upande wa maendeleo ya kiujenzi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako