• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Sudan Kusini athibitisha kuwa atasaini mkataba wa amani na waasi

    (GMT+08:00) 2018-08-04 19:06:06

    Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir amethibitisha kuwa yuko tayari kusaini mkataba wa amani wa mwisho na waasi siku ya jumapili katika mji mkuu wa Sudan Khartoum.

    Kiir aliyasema hayo wakati wa mazungumzo yake na waziri wa mambo ya nje wa Sudan, Al-Dirdiri Mohamed Ahmed ambaye yuko nchini Sudan Kusini kushuhudia utiaji saini wa awali kati ya serikali na upinzani kuhusu kugawana madaraka ya kiuongozi.

    Alisema pande zote mbili zilisaini mkataba wa amani mwaka 2015, licha ya kuwa ulipata changamoto kutokana mashinikizo ya jumuiya ya kimataifa yaliyosababisha kukwama kwake, lakini kwa sasa akisema kuna matumaini makubwa ya kufanikiwa kufuatia jitihada za usuluhishi zinazofanywa na Rais wa Sudan Omar Al-Bashir akishirikiana na IGAD.

    Pande hizo ziliingia kwenye mvutano Julai mwaka 2016 uliosababisha kiongozi wa waasi Riek Machar kukimbilia uhamishoni, na jambo hilo likazorotesha juhudi za IGAD za kutafuta amani ya Sudan Kusini, hivyo mazungumzo ya Khartoum kwa ajili ya mkataba wa amani huenda ikawa ndiyo nafasi ya mwisho kwa ajili ya amani ya Sudan Kusini.

    Endapo makabuliano yatafanikiwa, serikali ya mpito itakuwa na makamu wa Rais watano, Riek Machar akirejea katika nafasi yake ya makamu wa kwanza wa Rais, jambo ambalo Rais Salva Kiir amesema litafanikiwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako