• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkataba wa kugawana madaraka nchini Sudan Kusini kusainiwa mjini Khartoum

    (GMT+08:00) 2018-08-05 16:49:01

    Waziri wa mambo ya nje wa Sudan Al-Dirdiri Mohamed Ahmed jana ametangaza kuwa jumapili hii pande mbili zinazohasimiana nchini Sudan Kusini zinasaini mkataba wa mwisho wa kugawana madaraka ya kiutawala na uongozi mjini Khartoum.

    Waziri huyo amewaambia waandishi wa habari kuwa pande hizo hazitasaini mkataba kamili wa amani, kwa kuwa bado kuna baadhi ya vikundi vya upinzani nchini Sudan Kusini ambavyo bado vinatilia shaka, na kwamba majadiliano na vikundi hivyo yataendelea mjini Nairobi nchini Kenya.

    Wakuu wa nchi na serikali zilizopo kwenye mpango wa IGAD wanatarajiwa kuhudhuria hafla ya utiaji saini wa makubaliano hayo.

    Katika makubaliano haya ambayo ni ya awali, inaelezwa kuwa Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir ataendelea na wadhifa wake katika kipindi cha mpito, na kiongozi wa upinzani Bw. Riek Machar atarejea kwenye nafasi yake ya makamu wa kwanza wa Rais.

    Juhudi zote hizi, zinafanywa ili kutafuta suluhu ya kudumu katika nchi hiyo ambayo kumeshuhudiwa vita vya wenyewe kwa wenyewe tangu Disemba mwaka 2013 ambavyo vimepelekea vifo vya takribani watu 10,000 na wengine mamilioni kuyakimbia makazi yao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako