• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jeshi la Misri lawaua magaidi 52 huko Sinai

    (GMT+08:00) 2018-08-06 09:26:36

    Jeshi la Misri limetangaza kuwaangamiza magaidi 52 wenye hatari kubwa katika siku kadhaa zilizopita mkoani Sinai Kaskazini, ikiwa ni sehemu ya kampeni ya kupambana na ugaidi ya "Sinai 2018" inayoendelea.

    Magaidi hao walikuwa na bunduki nane, milipuko mitatu na risasi kadhaa. Msemaji wa jeshi hilo Bw. Tamer al-Refaie ametoa taarifa akisema, mashambulizi ya pamoja yaliyofanywa na jeshi na polisi yamesababisha kukamatawa kwa watu wengine 49 wenye msimamo mkali kaskazini na katikati ya Sinai.

    Ameongeza kuwa mashambulizi hayo pia yameharibu vituo na maghala 26 ya magaidi, na kuondoa milipuko 64 iliyovilenga vikosi hivyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako