• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • WHO yasema ugonjwa wa Ebola DRC ni hatari kwa taifa na kanda

    (GMT+08:00) 2018-08-06 09:33:49

    Shirika la Afya Duniani WHO limesema mlipuko mpya wa ugonjwa wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo unaleta hatari kubwa ya afya katika ngazi ya taifa na ngazi ya kanda, licha ya kuwa hatari yake kwa dunia ni ndogo sana.

    Mwanzoni mwa mwezi huu serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ilitangaza kuwa matokeo ya awali ya vipimo vya maabara yamethibitisha kuna virusi vya Ebola katika mkoa wa Kivu kaskazini. Hii ni zaidi ya wiki moja baada ya serikali hiyo kutangaza kwisha kwa mlipuko wa ugonjwa huo.

    Hadi kufikia ijumaa Agosti 3, matukio 43 ya ugonjwa wa Ebola yaliripotiwa, 13 yalithibitishwa kuwa ni maambukizi, na 30 yanadhaniwa kuwa ni maambukizi, na watu 33 kati ya hao wamefariki dunia. Wafanyakazi watatu wa afya wameambukizwa na wawili kati yao wamefariki.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako