• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Riadha, Kenya ndio mabingwa wa Afrika 2018: Washinda michuano ya Nigeria

  (GMT+08:00) 2018-08-06 10:20:13

  Licha ya changamoto ilizokumbana nazo katika safari ya kuelekea kwenye mashindano, timu ya taifa ya Kenya imefanikiwa kushinda nafasi ya kwanza kwenye mashindano ya riadha ya Afrika yaliyomalizika jana mjini Asaba nchini Nigeria.

  Kenya ambayo ilikuwa na jumla ya wanariadha 64 imeshinda nafasi ya kwanza baada ya kushinda medali 19, dhahabu 11, fedha 6 na shaba 2.

  Hii ni mara ya nne kwa Kenya kushika nafasi ya kwanza kwenye mashindano ya Afrika, ikiwa imewahi kufanya hivyo tena mwaka 1982 nchini Misri, 1984 nchini Tunisia na mwaka 2010 ilikuwa mwenyeji wa mashindano hayo.

  Mshindi wa pili kwenye mashindano ya Nigeria ni Afrika Kusini kwa kuwa na medali 30, dhahabu 9, fedha 13 na shaba 8 na wenyeji Nigeria wakiambulia nafasi ya tatu kwa kuwa na medali 19, dhahabu 9, fedha 5 na shaba 5.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako