• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa Sudan asisitiza kuunga mkono amani na utulivu nchini Sudan Kusini

  (GMT+08:00) 2018-08-06 19:55:18

  Rais Omar al-Bashir wa Sudan amesisitiza tena ahadi ya nchi yake kuunga mkono amani na utulivu nchini Sudan Kusini, na kufuatilia utekelezaji wa makubaliano ya amani yaliyosainiwa mjini Khartoum na pande zinazopingana nchini Sudan Kusini.

  Rais Al Bashir amesema mipango itaendelea kupangwa, miradi na ratiba ya kutekeleza kile kilichokubaliwa mjini Khartoum na kufuatilia hatua kwa hatua.

  Kwa upande wake, rais Salva Kiir wa Sudan Kusini ameapa kutekeleza makubaliano hayo kwa uhakika, na kusema kusainiwa kwa makubaliano hayo ni ishara ya kumalizika kwa mgogoro na vita nchini Sudan Kusini.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako