• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Gofu, Afrika: Uganda washinda ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati

    (GMT+08:00) 2018-08-07 08:31:27

    Timu ya taifa Uganda imefanikiwa kushinda kombe la ubingwa wa mashindano ya gofu ya Afrika kwenye kanda ya tano inayojumuisha nchi za Afrika Mashariki.

    Katika hatua ya fainali, Uganda waliishinda Rwanda ambayo ilifika hatua hiyo kwa kuifunga Kenya. Na Kenya walifanikiwa kushinda nafasi ya tatu baada ya kuwafunga Tanzania kwenye mzunguko wa kutafuta mshindi wa tatu.

    Mashindano hayo yalifanyika katika viwanja vya Gofu vya Nyali mjini Mombasa nchini Kenya na kuhudhuriwa na Rais wa chama cha mchezo wa gofu Duniani Kevin Weir.

    Timu nyingine zilizoshiriki michuano hiyo ni, Ethiopia, DRC, Burundi na shelisheli.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako