• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ongezeko la ajali za barabarani nchini Kenya lafanya usimamizi wa magari kufuatiliwa

    (GMT+08:00) 2018-08-07 09:26:52

    Ongezeko la idadi ya watu waliokufa kwenye ajali za barabarani nchini Kenya, limefanya tena suala la usimamizi wa magari kuanza kufuatiliwa tena.

    Kwenye ujumbe wa salamu za rambirambi kutokana na vifo vya wanafunzi kumi wa shule za msingi, Rais Uhuru Kenyatta amesema serikali itaimarisha sheria za usalama barabarani, ili kupunguza ajali kwenye barabara kuu.

    Viongozi mbalimbali wa Kenya wamesema ajali hiyo iliyotokea saa tano usiku, licha ya juhudi zinazofanywa na serikali kuboresha barabara na kuongeza polisi wa usalama barabarani, imethibitisha kuwa bado kuna hatari kwenye usafiri wa barabara nchini Kenya.

    Ajali hiyo ilitokea baada ya basi lililokuwa linasafirisha wanafunzi kutoka Mombasa, kugongana na lori, lililokuwa limepoteza mwelekeo mteremkoni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako