• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania kupanga madaraja ya hoteli mjini Dodoma

    (GMT+08:00) 2018-08-07 09:27:16

    Tanzania itaanza hivi karibuni mchakato wa kuweka madaraja ya hoteli na nyumba za wageni mjini Dodoma, wakati kasi ya serikali kuhamia Dodoma ikiendelea kuchukua kasi.

    Katibu mkuu wa Wizara ya Utalii na Maliasili ya Tanzania Bw. Gaudence Milanzi, amesema lengo la hatua hiyo ni kuhakikisha kuwa hoteli zinatoa huduma bora, wakati idara za serikali na ofisi za kibalozi zinahamia Dodoma.

    Bw. Milanzi amesema mji wa Dodoma unatarajiwa kupokea ujio wa watu wengi, na kufanya kuwe na haja ya kuongeza na kuboresha hoteli ili kukidhi mahitaji ya watu. Mbali na kuweka madaraja kwenye hoteli, Bw. Milanzi ameelezea umuhimu wa kuboresha sekta ya huduma mjini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako