• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uhusiano kati ya Canada na Saudi Arabia wazorota

    (GMT+08:00) 2018-08-07 09:30:27

    Waziri wa mambo ya nje wa Canada Chrystia Freeland amesema nchi hiyo siku zote inatetea haki za binadamu, na haitalegeza msimamo unaosababisha mzozo wa kidiplomasia na Saudi Arabia.

    Ijumaa iliyopita, wizara ya mambo ya nje ya Canada ilisema nchi hiyo ina wasiwasi na kukamatwa kwa wanaharakati wa asasi za kiraia na haki za wanawake nchini Saudi Arabia, na kutaka serikali ya Saudi Arabia iwaachie huru mara moja watu hao na wanaharakati wengine wote wa haki za binadamu. Wakati huohuo, wizara ya mambo ya nje ya Saudi Arabia imeishutumu Canada kwa kuingilia mambo ya ndani ya nchi hiyo, na kutangaza kusimamisha makubaliano yote mapya ya biashara na uwekezaji na Canada na kutaka balozi wa Canada nchini humo aondoke ndani ya saa 24.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako