• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • UNICEF yasaidia kuachiwa huru kwa askari watoto Sudan Kusini

  (GMT+08:00) 2018-08-07 19:24:10

  Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) limesema askari watoto 128 wameachiwa huru kutoka makundi ya waasi yaliyovunjwa huko Yambio, mkoa wa Western Equatoria kusini mwa Sudan Kusini.

  Katika taarifa yake iliyotolewa leo, Shirika hilo limesema watoto 90 wa kiume na 38 wa kike wameachiwa huru kutoka makundi ya SSNLM na kundi la SPLA-IO, hivyo kufanya kundi la nne la watoto walioachiwa huru tangu mapigano yaanze mwezi Disemba mwaka 2013. Watoto hao walinyang'anywa silaha zao na kupewa mavazi ya kiraia, na kwamba uchunguzi wa afya zao utafanyika. Pia watoto hao watapewa ushauri nasaha na msaada wa kisaikolojia ikiwa ni sehemu ya mradi wa kuwarudisha tena katika jamii.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako