• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Botswana yaahidi kuimarisha uhusiano wa kirafiki na China

    (GMT+08:00) 2018-08-08 09:32:27

    Msemaji wa serikali ya Botswana Bw. Jeff Ramsay amesema, nchi hiyo imeahidi kuimarisha uhusiano wa pande mbili na China wakati rais Mokgweetsi Masisi atafanya ziara nchini China mwezi ujao.

    Bw. Ramsay amesema rais Masisi anatarajiwa kuongoza ujumbe wa Botswana kuhudhuria mkutano wa kilele wa baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC utakaofanyika mwezi ujao jijini Beijing.

    Kwa mujibu wa Bw. Ramsay, rais Masisi ameahidi kuimarisha urafiki na ushirikiano kati ya Botswana na China juu ya msingi wa pande mbili na nyingi. Rais Masisi atakuwa rais wa kwanza wa Botswana kufanya ziara rasmi nchini China katika miaka 12 iliyopita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako