• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Soka, Mechi za Kirafiki: Simba ya Tanzania kucheza na Asante Kotoko ya Ghana

  (GMT+08:00) 2018-08-08 09:42:12

  Leo jioni mjini Dar es Salaam nchini Tanzania, timu ya Simba inacheza mechi ya kirafiki dhidi ya mabingwa mara 24 wa ligi kuu nchini Ghana timu ya Asante Kotoko.

  Mechi hii ni sehemu ya maadhimisho ya wiki maalum ya klabu ya Simba ambayo kila mwaka ifikapo Agosti mosi klabu hiyo husherehekea kwa muda wa juma zima na kilele cha maadhimisho ni Agosti 8.

  Asante Kotoko ambayo ilitajwa kuwa miongoni mwa klabu 6 maarufu duniani za karne ya 20, iko nchini Tanzania tayari kwa ajili ya mechi hiyo.

  Siku ya kilele cha maadhimisho hayo (Simba Day) hutumika pia kutambulisha kikosi cha wachezaji wa simba kilichoandaliwa kwa ajili ya msimu mpya wa ligi kuu Tanzania Bara.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako