• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mpira wa Wavu, Wanawake: Kenya wakanusha uvumi kuwa nusu ya wachezaji timu taifa wana ujauzito, pia itashiriki kombe la dunia

  (GMT+08:00) 2018-08-08 09:44:03

  Shirikisho la mchezo wa mpira wa Wavu la nchini Kenya KVF, limekanusha taarifa zilizozaga kwenye majukwaa mbalimbali ya mtandao wa Internet, kwamba timu ya taifa ya wanawake haitashiriki michuano ya kombe la Dunia ya mwaka huu kwa kuwa nusu ya wachezaji wake ni wajawazito.

  Katika taarifa hiyo ya kukanusha, KVF imesema timu hiyo itashiriki michuano tajwa ya kombe la dunia na kwamba si kweli kuwa nusu ya wachezaji wana ujauzito, na kuhusu baadhi ya wachezaji ambao hawajajumuishwa kwenye kikosi kilichoteuliwa ni kwa sababu mbalimbali ikiwemo majeruhi.

  Michuano ya kombe la dunia ya mchezo wa mpira wa wavu wanawake inatarajiwa kufanyika nchini Japan mwezi ujao ambapo jumla ya timu 24 zinashiriki, na Kenya ni moja ya timu mbili pekee zinazoliwakilisha bara la Afrika ikiwa pamoja na timu ya taifa ya Cameroun.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako