• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mchumi mkuu wa IMF asema ni kosa kwa Marekani kujaribu kupunguza urari wa biashara kwa njia ya kuongeza ushuru

  (GMT+08:00) 2018-08-08 16:17:01

  Mchumi mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa IMF Bw. Maurice Obstfeld amesema ni kosa kwa Marekani kujaribu kupunguza urari wa biashara kwa njia ya kuongeza ushuru wa forodha.

  Bw. Obstfeld ameeleza wasiwasi mkubwa juu ya uelewa mbaya wa serikali ya Marekani kuhusu urari wa biashara, ambao huenda utasababisha kutungwa kwa sera nyingi zaidi za kujilinda kibiashara, hatua ambayo si kama tu haitasaidia kutatua ukosefu wa uwiano wa biashara duniani, na bali pia itachochea zaidi mgogoro wa kibiashara na kuhujumu ukuaji wa uchumi wa dunia.

  Takwimu zilizotolewa hivi karibuni na wizara ya biashara ya Marekani zinaonesha kuwa katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, urari mbaya wa biashara ya bidhaa na huduma za Marekani ulifikia dola za kimarekani bilioni 29.12, ikiwa ni ongezeko la asilimia 7.2 kuliko mwaka jana wakati kama huo na kuthibitisha kuwa kuongeza ushuru wa forodha hakuwezi kupunguza urari wa biashara.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako