• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mpira wa Wavu: Viongozi wa Chama cha watu wenye Ulemavu wajiweka sawa kwa mpira wa wavu

  (GMT+08:00) 2018-08-09 08:46:45
  Chama cha watu wenye ulemavu wa viungo Zanzibar wamefunga mafunzo maalum ya mchezo wa mpira wa wavu wa kukaa (Volleball siting) kwa watu wenye ulemavu Zanzibar yaliyofanyika kwenye viwanja vya Amani mjini Unguja.

  Hassan Haji Silima Mwenyekiti wa michezo kwa watu wenye ulemavu wa Viungo Zanzibar amesema mafunzo hayo yana lengo la kuwapa mafunzo viongozi wa watu wenye ulemavu wa viungo kutoka kwenye wilaya ili kuhakikisha mchezo huo unachezwa katika kila wilaya.

  Aidha ametoa wito kwa jamii kufahamu umuhimu wa michezo kwa watu wenye ulemavu wa Viungo Zanzibar kwa kuwa michezo hiyo huchezwa kimataifa kwa sasa na kutaka wadau wa michezo kukiunga mkono chama cha chao kwa kuwa kina malengo ya kuitangaza Zanzibar kwenye mchezo huu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako