• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mlipuko wasababisha askari 6 kujeruhiwa nchini Kenya

    (GMT+08:00) 2018-08-09 09:23:34

    Askari zaidi ya 6 wa jeshi la Kenya KDF wamejeruhiwa katika shambulizi linaloshukiwa kufanywa na kundi la al-Shabab mjini Lamu. Msemaji wa KDF Bw. Paul Njuguna amesema, askari hao walikuwa wanafanya doria ya kawaida, wakati gari lao linakanyaga bomu.

    Watatu kati yao wako katika hali mbaya, na wamesafirishwa kwa ndege ili kwenda kupatiwa matibabu maalumu. Majeruhi wengine wanaendelea vizuri.

    Serikali ya Kenya imekuwa inafanya operesheni inayoitwa linda Boni yenye lengo la kuwafurusha wapiganaji wa kundi la Al Shabaab kutoka msitu wa Boni, ambao inaaminika kuwa wanautumia kupanga mashambulizi yao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako