• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kampuni ya Alibaba yazindua mpango wa kusaidia vijana wajasiriamali wa Afrika

    (GMT+08:00) 2018-08-09 10:51:32

    Mkuu wa Kampuni ya Alibaba ya China Bw. Jack Ma amezindua tuzo ya kuwaunga mkono viongozi wafanyabiashara wa nchi za Afrika. Tuzo hiyo yenye thamani ya dola milioni 10 za kimarekani, itatolewa kwa wajasiriamali 100 wa Afrika katika miaka 10 ijayo, ili kusaidia uvumbuzi mashinani, kuwawezesha kiuchumi wanawake na biashara ndogondogo.

    Akiongea mjini Johannesburg, Bw. Jack Ma amesema tuzo hii inaonyesha uungaji mkono wa kampuni ya Alibaba kwa wajasiriamali vijana wa Afrika wanaoandaa mazingira kwa ajili ya vizazi vijavyo, na kuleta mabadiliko chanya kwenye jamii.

    Bw. Jack Ma amesema amepata hamasa ya kuanzisha tuzo hiyo baada ya kutembelea bara la Afrika kwa mara ya kwanza mwaka jana, na kujionea nguvu na uwekezano wa ujasiriamali kwa vijana aliokutana nao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako