• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa wasema rais wa DRC kutogombea tena katika uchaguzi mkuu ni maendeleo

    (GMT+08:00) 2018-08-09 15:40:52

    Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameutaja uamuzi wa rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kutogombea tena katika uchaguzi mkuu kuwa ni "maendeleo".

    Msemaji wa katibu mkuu huyo Farhan Haq amesema wamepokea taarifa kuwa Emmanuel Ramazani Shadary ameteuliwa kama mgombea wa muungano wa chama tawala kuwa mgombea urais katika uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Disemba 23 mwaka huu.

    Uteuzi wa Shadary kama mgombea nafasi ya urais umemaliza miezi kadhaa ya uvumi kuhusu hatma ya baadaye ya rais Kabila, ambaye muhula wake wa mwisho ulimalizika mwishoni mwa mwaka 2016.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako