• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kuimarisha urafiki kati ya China na Afrika ni ajenda muhimu ya diplomasia ya China kwa mwaka huu

    (GMT+08:00) 2018-08-09 16:59:54

    Mwezi ujao mkutano wa kilele wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika utafanyika hapa Beijing, ikiwa ni shughuli nyingine muhimu ya kidiplomasia ya China. Katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, shughuli nyingi za kidiplomasia kati ya China na Afrika zimefanyika, na viongozi wa China na nchi za Afrika wametembeleana, hali inayothibitisha urafiki mkubwa uliopo kati ya pande hizo mbili.

    Tarehe 22 mwezi Machi mwaka huu kwenye jumba la mikutano la watu wa China hapa Beijing, rais Xi jinping alimkaribisha mwenzake wa Cameroon Bw. Paul Biya, ambaye mgeni wake wa kwanza tangu achaguliwe tena kuwa rais wa China. Rais Xi anasema,

    "Cameroon ni nchi rafiki wa jadi wa China na mwenzi muhimu wa ushirikiano barani Afrika. China inapenda kushirikiana na Cameroon, kuenzi urafiki huo mkubwa, kupanua ushirikiano wenye mustakbali mkubwa kati ya nchi mbili, na kuusukuma mbele uhusiano wa nchi mbili ufikie ngazi mpya, ili kuwanufaisha zaidi watu wa nchi hizo mbili."

    Baada ya rais Biya, marais wa Namibia na Zimbabwe pia walifanya ziara nchini China. Ziara hizo za viongozi wa nchi za Afrika zimekuja miaka mitano baada ya rais Xi Jinping kutoa mtizamo wa sera ya Afrika unaozingatia ukweli, uhalisi, ukarimu na udhati.

    "Tunawatendea marafiki zetu wa Afrika kwa ukweli, kufanya ushirikiano na nchi za Afrika kwa uhalisi, kuimarisha urafiki wa China na Afrika kwa ukarimu, na kutatua masuala yaliyopo kwenye ushirikiano wetu kwa udhati."

    Kama alivyofanya miaka mitano iliyopita, rais Xi Jinping aliyechaguliwa tena kuwa rais wa China amefanya ziara yake ya kwanza barani Afrika, ambayo ni ziara yake ya nne barani humo tangu aingie madarakani. Akiwa nchini Senegal, ambayo ni kituo cha kwanza cha ziara yake, rais Xi alisema,

    "Kila mara ninapokuja Afrika naweza kuhisi kwa kina uhai na uchangamfu wa bara hili. Watu wa Afrika wanatarajia maisha bora na bara la Afrika limeonesha mustakbali mkubwa wa maendeleo. Maendeleo ya China yatatoa fursa nyingi kwa Afrika, na maendeleo ya Afrika pia yatatia nguvu maendeleo ya China, nina imani kubwa na ushirikiano kati ya China na Afrika."

    Kinachobeba matarajio hayo makubwa kwa uhusiano kati ya China na Afrika, ni mipango mbalimbali ya ushirikiano. Katika miaka mitatu iliyopita, akihutubia ufunguzi wa Mkutano wa kilele wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC mjini Johannesburg, rais Xi Jinping aliahidi kutekeleza mipango kumi mikubwa ya ushirikiano kati ya China na Afrika katika miaka mitatu ijayo, ambayo imeitikiwa mara moja na nchi mbalimbali za Afrika. Rais Thomas Boni Yayi wa Benin alisema,

    "Katika mazingira ya kimataifa ambayo uchumi wa dunia unadidimia, China bado inaendelea kuisaidia Afrika, na kuitendea kama rafiki mkubwa. Ni kutokana na kuwa na rafiki huyo, Afrika imekuwa na imani zaidi kukabiliana na changamoto zijazo."

    Mwanzoni mwa mwaka huu, waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi alifanya ziara katika nchi nne za Afrika, Malawi, Mauritius, Msumbiji na Namibia, kwa lengo la kutekeleza mipango hiyo ya ushirikiano iliyotolewa na rais Xi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako