• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkuu wa UNICEF ashtushwa na shambulizi la anga lililolenga basi la shule kaskazini mwa Yemen

    (GMT+08:00) 2018-08-10 09:33:15

    Mkuu wa Shirika la kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF Bibi Henrietta Fore amelaani shambulizi la anga dhidi ya basi la shule lililotokea jana katika eneo la kaskazini mwa Yemen, ambalo linaripotiwa kuwaua watoto zaidi ya 24, wengi wao wakiwa na umri wa chini ya miaka 10.

    Bibi Fore ametoa wito kwa pande zote zinazopambana kuheshimu sheria ya kibinadamu ya kimataifa na kuwahurumia watoto, raia na miundombinu ya kiraia, ili kuzuia Yemen isitunbukie zaidi kwenye lindi la maafa ya kibinadamu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako