• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kikundi cha madaktari wa China chaipatia hospitali ya Uganda vifaa vya matibabu

    (GMT+08:00) 2018-08-10 09:44:03

    Kikundi cha 18 cha madaktari wa China nchini Uganda kimefanya hafla ya kuipatia Hospitali ya Naguru dawa na vifaa vya matibabu mjini Kampala.

    Balozi wa China nchini Uganda Bw Zheng Zhuqiang amehudhuria hafla hiyo, na kusema, China na Uganda zimekuwa na ushirikiano wenye ufanisi kwenye sekta ya afya ya umma, na hatua zaidi za ushirikiano zinatarajiwa kutolewa katika mkutano wa kilele wa baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika utakaofanyika Beijing mwezi ujao. Ametaka China na Uganda ziendelee kuimarisha ushirikiano kwenye sekta ya afya ya umma kwa kutumia fursa hiyo.

    Waziri wa afya wa Uganda Bibi Jane Aceng ameishukuru China kwa msaada wake katika sekta ya afya nchini Uganda. Amesema dawa na vifaa vya matibabu vinavyotolewa na China vitasaidia kutatua uhaba wa dawa katika Hospitali ya Naguru.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako